‘’Sisi hatutamkumbatia kamwe adui wetu hapa.’’ Lt Kanali Mutembe.

Luteni Kanali Frank Mutembe ambaye ni mkuu wa majeshi ya Rwanda Wilayani Gasabo, Mjini Kigali wakati alipojiunga na wakazi wa Wilaya ya Gasabo katika hatua ya kijamii ‘Umuganda’’, yeye alisema kuwa watu wanaotaka kuvuruga usalama wa Rwanda hawana nafasi.

‘’ nataka nyinyi kutusaidia kwa kujua ni nini kinachojificha katika nyumba zinazo baki kufungwa kila siku, ndugu, viongozi, vijana mtuusaidie kujua hivyo kisha mtoe habari…ni jukumu letu kuwazuia watu kama hao. Sisi hatutakubali kumkumbatia adui hapa.’’ Mutembe alisema.

Watu wanoua ndugu zao kwa sababu ya dini, hawa watu wanasaka vijana wadogo kwa kuwafunza kujilipua, hilo ni jambo tunalosikia nchini Syria lakini watu kama hao nchini Rwanda hawana nafasi.

Hawa watu ni lazima kulazimishwa kuachana na itikadi ya ugaidi kwani usalama ndicho kitu muhimu Rwanda humiliki.

Lt Kanali Frank Mutembe alisema hayo baaka ya watu nne (mmoja mjini Kigali/Nyarutarama na wengine watatu Wilayani Rusizi/Bugarama, magharibi mwa Rwanda.) kuuawa na jeshi la Polisi wakishtakiwa kuwa magaidi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments