Wizkid anaanza shoo yake ya kwanza mjini Kigali

Wizkid
Muimbaji mashuhuri wa Nijeria Wizkid alifika Rwanda jana asubuhi ambako alipokelewa kifalme.

Katika mahojiano na wandishi wa habari, Huyo staa alisema kwamba yeye hakukuja kuimba tu, yeye aliambia wanahabari kuwa alikuja kujionea uzuri wa wasichana wa Rwanda kwani yeye aliambiwa na Davido na mastaa wengi wa Nijeria waliotembelea kwamba wako wasichana wazuri nchini Rwanda.

Wizkid anatarajia kutumbuiza ndani ya ukumbi wa Kigali Convention Center leo hii na Rugende training ceneter siku ya jumamosi.

Wizkid amekuwa nchini Tanzania kabla ya kutua Rwanda jana jumatano.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments