Dk Rose Mukankomeje anarudi mbele ya sheria.

Aliyekuwa mkuu wa mamalaka ya kusimamia mazingira nchini Rwanda Dk Rose Mukankomeje anatarajiwa kupandishwa mahakamani tena ili kujibu makosa anayoshtakiwa kutenda akitumia nafasi ya kazi.

Mukankomeje aliachiwa na mahakama makuu kwa muda tarehe 14, Aprili , 2016 baada ya kutiwa nguvuni tarehe 21 mwezi Machi ,2016. Bi. Mukankomeje yuko mikononi mwa sheria kwa tuhuma za mazungumzo aliyoyafanya kwenye simu ya mkononi na Bisamaza Prudence aliyefuatiliwa uhalifu wa rushwa na kuvunja siri ya kazi.

Uendesha mashtaka wa Rwanda unamesema kwamba wao wamechukulia kesi ya Mukankomeje katika mahakana ya msingi ya Kagarama ili aanze kujibu mashtaka yake kwa kina.

Emmaneul Itamwa ambaye ni msemaji wa uendesha mashtaka anasema kuwa Mukankomeje anatarijia kupandishwa mahakamani tarehe 27, mwezi tisa, 2016

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments