Je, wivu ni ishara ya mapenzi !

Wivu ni ishara kubwa sana ya kugundua kuwa mpenzi wako anakupenda kwa dhati. Sidhani kama kuna mtu asiye na wivu, ila tunatofautiana, wapo watu wanaouonyesha dhahiri na wengine huuficha, lakini wanaumia kwa ndani.

Wivu si kipimo cha mapenzi ila kujiheshimu ndio kipimo cha mapenzi. Mapenzi bila wivu si mapenzi hayo. Ramadhan Mkindi wa Arusha. Wivu ukizidi sana matokeo yake ni ugomvi.

Kutokana na hali ya mahusiano ilivyo kwa sasa, thamani ya mapenzi imeisha ladha, kwa kweli wivu ni muhimu kwenye mahusiano, ni ishara ya upendo kwa mwenza wako.

Mtu mwenye wivu ndio mzuri, maana anatambua umuhimu wa mapenzi ndani ya watu wawili mnaopendana, pia mtu huyu mwenye wivu anaonyesha ni jinsi gani anavyokupenda si yule ambaye hamjali mtu wake. Bernard Kilala.

Wivu ni kiungo muhimu sana katika mapenzi, kama hakipo hata upendo haupo, endapo mmoja wa wapenzi atadharau huduma ya kiungo cha wivu katika mapenzi, jua hajui hata maana ya mapenzi, hata neno lenyewe penzi ajifunze.

Mapenzi si mate kila mtu ayapate, ninasema hivyo kwa sababu wivu ni ishara tosha ya kujua jinsi gani unampenda mwenzi wako, kwa asiyejua thamani ya mapenzi hawezi kumuonea wivu mwenzake. Wamwisho Kufa, Nevada Salon, Buguruni Sheli, Dar es Salaam.

Wivu katika mahusiano ni alama ya upendo kwa sababu mmoja kati yenu akionyesha wivu anakukinga na hatari ambayo ingeepukika. Kama mwenza wangu akionyesha wivu, najua ananipenda na ananilinda na vishawishi.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments