Mabasi ya umma yavunja rikodi ya kusababisha vifo vya watu- Ripoti

1

Jeshi la Polisi nchini Rwanda, katika ripoti yao, linasema mabasi ya abaria yanaripotiwa kuwa ya kwanza kusababisha vifo vya watu barabarani.

Katika mkutano na wamiliki na wakilishi wa makampuni ya usafiri uliofanyika kwenye makao makuu ya jeshi la polisi jijini Kigali jana tarehe 24 Agosti 2016, Kamishna wa polisi George Rumanzi ambaye ni kamishina mkuu wa idara ya usalama wa kitaani alisema kwamba mabasi yanayosafirisha abiria yamesababisha vifo vya watu 408 na wengine 91 kujeruhiwa.

Na Kamishna huyo alibaini kwamba madereva walevi, mwendo kasi wa mabasi, kuongea kwenye simu madereva wakiongoza magari ndio chanza cha ajali.

Kamishina mkuu wa jeshi la polisi ( IGP ) Emmanuel Gasana alisema « Rwanda ni nchi inayopiaga hatua katika ngazi tofauti, kunatakiwa magari ya abiria ya kutosha. Tunawakaribisha wageni wengi kwa shughuli za utalii na utalii wa kimataifa, nyie makampuni husika mnapaswa kutoa huduma bora kwa wageni hao ».

Aliwakumbusha pia kuweka mikakati kabambe katika makampuni yao ili kuboresha shughuli na kupiga hatua kimaendeleo na kujulinda ajari barabarani.

Makamu wa meya wa mji Kigali Busabizwa alisema “Malighafi ya Rwanda ni wananchi, ndiyo sababu tunapaswa kuwalinda kila kukicha, ulevi wa madereva ni chanzo muhimu cha ajari barabarani”.

Mwakilishi wa Rwanda Federation of Transport Cooperatives (RFTC) Kanali mstaafu Ludovic Twahirwa alisema “Hatuwezi kupatia kibarua dereva bila agizo la mtumishi wake wa zamani kwani anaweza kufutwa kazini kwenye kampuni ya kwanza kwa sababu ya utovu wa adhabu na kuajiriwa kwenye kampuni nyingine. Hili ni tatizo la kutafutiwa tiba punde si punde”.

Mkutano huu umeamua kuweka vifaa vitakavyopima kasi ndani ya magari ya abiri, usajiri wa madereva na kupewa vitambulisha vya kazi.


Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

  1. hizi accident zinatisha sana vilevile watu wameanza ogopa
    safari mbalimbali tafaut kwasababu ya hizi accident
    RTFC
    itafute solution ya hili tatizo tunaamini wataweza !.

Tumia Comments