Waziri amuita Kagame ’Baba wa taifa’.

Kote duniani kila nchi ina mtu aliyekuwa rais katika miaka ya zamani tangu nchi kuundwa au kupata uhuru wake, mtu huyo kutokana na sifa zake wakati alikuwa madarakani.

Huu kigogo wa siasa nchini kwake na hata duniani kote ni mtu ambaye hawezi kusahaulika katika historia ya nchi, na wananchi wanapenda kumuita ‘Baba wa taifa au Father of the nation in English.

Kwa hivyo, Sheikh Musa Fazil Harerimana, waziri wa usalama wa ndani na ni mkuu wa chama cha kidemokrasia bora (PDI) anasema kwamba bila shaka, Rais Paul Kagame anastahili kuitwa baba wa taifa kama Nelson Mandela wa Afrika kusini na George Washington wa Marekani kwani Paul Kagame ni Rias wa kwanza miongoni mwa marais walioongoza Rwanda ambaye alifanikiwa na kuweka siasa bora ambayo marais wengine ambao wataongoza Rwanda wanapaswa kufuata.

Katika mahojiano na Igihe kuhusu maandalizi ya kumchagua mgombea urais mwaka ujao wa 2017, Harerimana amesema kwamba Chama chake hakiwezi kumtafuta mwingine, yeye anasisitiza kuwa mgombea wao wameisha kumuonesha wakati wao walitaka katiba ya Rwanda kubadilika ili kumruhusu Kagame kuwania muhula mwingine baada ya miaka 14 kumalizika akiwa madarakani.

Fazil alibaini kuwa Rais Paul Kagame ni mtu ambaye atakumbukwa katika historia ya Rwanda, tulimchagua kuwa mgombea wetu tangu mwaka wa 2010 na sisis hatutafanya mkutano mwingine wa kumchagua mgombea urais.

‘’ sisi, wanachama wa PDI katika mwaka wa 2010, mgombea wetu alikuwa Kagame. Kwa hiyo sisi hatukuchagua mwingine katika mkutano mkuu wa PDI. Tuliita wanyarwanda kubadili katiba ili Kagame aendelee kuongoza Rwanda. Kisha Wananchi walikubali mwito wetu, hii inamaanisha kuwa Kagame ni mgombea wetu, hakuna mwingine.’
’ Sheikh Fazil alisema.

Harerimana aliendelea kusema kwamba chama tawala FPR hakiwezi kumuacha Kagame bila mpango, ikiwezekana RPF kutomchagua Kagame kuwa mgombea urais , PDI pia itaanza kampeni za kumchagua mgombea ambaye atawakilisha chama hicho katika mbio za kumsaka Rais.

Kwa jina la wanachama wa PDI, Fazil anasema kwamba Kagame ni kingozi aliyejengea Rwanda kwa wanyarwanda bila ubaguzi wa kiala aina, kwa hivyo, Kagame ni Rais ambaye atakumbukwa katika historia ya Rwanda.

‘’hakuna mtu anayestahili kiti cha urais kuliko Kagame. Yeyote ambaye atakuwa Rais wa Rwanda baada ya Kagame, Mtu huyo anapaswa kufuata siasa ya Kagame. Katika kila nchi kuna mtu anayesifiwa kuwa ‘baba wa taifa’, mtu huo nchini Rwanda, ni Rais Paul Kagame.’’ Fazil aliongeza.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments