DRC : Mauaji ya Kanali Elias Byinshi yaibua maswali mengi

1

Kanali Elias Byinshi alitajwa katika kesi ya mauaji ya Mutarule. Hapa makaburi ya wahanga (picha ya zamani).

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Kanali Elias Byinshi alizikwa Jumatano Agosti 24. Afisa huyu wa jeshi la Congo aliuawa mwishoni mwa wiki iliyopita katika mji wa Bukavu, siku chache baada ya kesi ya mauaji ya Mutarule.

Kanali Elias Byinshi alitajwa katika kesi hiio, akishtumiwa kushindwa kulinda waathirika, huku kukiwa na mgogoro kati ya jamii ya Banyamulenge na Bafulero. mauaji haya yameibua maswali mengi na hofu katika mkoa wa Kivu ya Kusini.

Katika siku iliyofuata mauaji ya afisa huyo, hali ya sintofahamu ilishuhudiwa katika mji wa Bukavu. Mauaji ya afisa wa jeshi kutoka jamii ya Banyamulenge yamezua hofu na uwezekano wa kutokea tena machafuko mapya katika bonde la Rusizi ambapo jamii ya Banyamulenge na Bafulero zimekua mara kwa mara katika migogoro kwa zaidi ya miaka 20.

Kanali Elias Byinshi aliyetumwa katika bonde la Rusizi mwaka 2014, alikuwa akishtumiwa na jamii ya Bafulero kuhusika katika mauaji ya watu kadhaa kutoka jamii hiyo katika kijiji cha Mutarule. "Alitakiwa kuripoti mahakamani, lakini alipinga agizo hiloi," chanzo cha kijeshi kimesema.

Umoja wa Mataifa uliwahi kuishinikiza serikali ya Congo kumfuta kazi bila mafanikio. Kabla ya kifo chake, Kanali Elias Byinshi aliandama na baadhi ya watu kutoka jamii ya Banyamulenge katika baa moja. Jioni alipokua akirudi nyumbani kwake aliuawa kwa risasi, licha ya kuwepo kwa mlinzi.

Chanzo : RFI

Changia hii habari na wenzako.

Comments 1

  1. , lakini kupenda na siko kupenda hatutatoka mulenge kizuri tuishi wote kama sivyo nyinyi mutahama sijui fasi muritayarisha masasi yatalamukiya siku moja x njo final

Tumia Comments