Gakenke : Anyang’anywa mtotowe baada ya kujifungua

Nzamwitakuze Brigitte ni mzazi na mkazi wa kata ya Coko kijijini Nyange katika kiini cha Karambo ambaye alifungua mototo mvulana tarehe 22 Agosti 2016 katika hospitali ya Ruli wilayani Gakenke.

Mtoto huyo aliperekwa mahali pekee ili asaidiwe kama ipasavyo, baada ya masaa machache Nzamwitakuze alikatishwa tama na habari aliyoiambiwa kuwa mtotowe alifariki dunia.

Shufaka ilijaa moyoni mwa familia hiyo baada ya kujua kifo cha mwanao na kujianda mazishi pia waganga walimpa sanduku (kifaa wawekacho mototo aliyefariki).

Walipigwa na butwaa wakati walipofungua sanduku na kukuta mototo laghai na mawe ndani humo, bila kusita wazazi hao waliamua kuita uongozi na walinda usalama ili wawaonyeshe balaa wanayoiona.

Akiongea na Makuruki, katibu mtendaji wa kata ya Ruli Habanabakize Jean Claude alisema “Tulishikwa na butwaa na huruma, tulifanya upererezi na kumushika nguvuni mshukiwa mganga Bucyensenge Beatha mwenye umri wa miaka 28 alietekeleza kuweka matendoni mpango huo wa kinyama. Mshukiwa huyo alituambia kuwa alikuwa alimhitaji mtoto baada ya miaka miwili bila kujifungua kwani alifunga ndoa 2014”.

Kwa usasa, mototo huyo ako katika hali nzuri na wazazi we walimchuku nyumbani, uongozi unasema kuwa hakukuwa na ugomvi wala tatizo kati ya mshukiwa na mzazi huyo.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments