Punde si punde, Kanyankore Gilbert aoneshwa mlango !

Baada ya siku nne kupewa majukumu kama makocha wa timu ya taifa (Amavubi) Kanyankore Gilbert Yaounde na Eric Nshimiyimana wametimuliwa na wizara ya utamaduni na michezo.

Tarehe 19 Agosti 2016 baada ya kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha wa timu ya taifa McKinstry makocha hao ndipo walipewa timu hii ili waisaidie katika siku hizi kwa kujiandaa mechi dhidi Ghana.

Ikumbukwe kwamba, waliweka hadharani orodha ya wachezaji 26 tarehe 22 Agosti 2016 ambao watacheza mechi ya kuwania na kukatisha tiketi ya kucheza michezo ya CAN itakayochezewa nchi Gabon mwaka kesho ingawa timu ya taifa haina tumaini ya kushiriki katika mshindano hayo.

Katika mahojiano na gazeti la Izubarirashe Kanyankore alisema kuwa wizara ya utamaduni na michezo (MINISPOC) ndiyo iliyochukua uamuzi huo mkali unaokuja kighafla. Tumejaribu kupigia simu uongozi wa MINISPOC lakini hawakupakupatikani kwenye laini ya simu.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments