Gasabo : Walalamikia fujo, usherati na ulevi

Wakazi wa kijiji cha Nyagatovu katika kata ya Kimironko wilayani Gasabo katika maeneo kwa jina maarufu ’Mukubite umwice’ wanalalamikia na kuzidiwa na fujo, wizi, ulevi na ukahaba ambavyo husababisha uhaba wa usalama.

Katika majohiano na wakazi wa maeneo hayo ambao waliambaia MAKURUKI kwamba chanzo cha fujo hiii ni ulevi kwani walevi wanapigana wengine kufanya ukahaba, ulevi huo husababishwa na pombe ikiwemo pombe maarufu kwa jina surudiwili.

Mkazi wa maeneo hayo ambaye hakutaka kutaja jina lake kwa sababu ya usalama alisema “Waweza kulemaa viungo vya mwili kwa sababu ya kupigwa, chanzo ni ulevi wa wakati wa huku kwa sababu ya pombe hii (surudiwili), kingine ambacho tunaona ni tatizo kubwa ni usherati”


“Nilikuta tatizo hili la usherati, fujo, vurugu wakati nilipofika hapa 2011, walimpiga mlinda amani wakati alipokuja kumtafuta malaya, ukifika hapa kama saa nane usiku unaweza kupigwa na butwaa na kutuonea huruma kwani hatulali wala kusinzia kwa sabau ya kelele na fujo”
. Alisema mkazi mwingine

Katibu mtendaji wa kata ya Kimironko Karamuzi Godfrey alisema “Tulishirikiana na jeshi la polisi, wanajeshi, siku zilizopita tulifanya oparesheni walifunga baa nyingi na kushauri wanawake Malaya, kwa usasa natuma Dasso kusaka watu wasio na utambulisho”

Kuhusu kumbo la wananchi katika maeneo haya ( High risk zone), katibu mtendaji alisema kwamba kuna mpango wa kuwahamisha katita maeneo hayo kwani ni mojawapo ya chanzo cha fujo hilo pia kuda nyumba za kodi ya bei ya chini.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments