Kodi ni ngao muhimu ya kupiga hatua kimaendeleo “Waziri mkuu Murekezi”

Waziri mkuu wa Rwanda Anastase Murekezi alisema kwamba wanyarwanda wakiendelea na utamaduni wa kulipa ushuri na kodi bila shaka Rwanda itakuwa na maendeleo ya kudumu kwani mataifa yaliyopiga hatua kimaendeleo ni nguvu za wananchi kupitia ushuri.

Waziri Murekezi aliwakumbusha wanyarwanda kuwa hakuna nchi inayoweza kujiendeleza bila ushuri kwani miundo mbinu ni nguvu za ushuru wa wananchi.

“Tunajivunia kwamba wanyarwanda walisikia vizuri destruri ya kujiendeleza bila kutegemea fimbo ya mbali kupitia kodi, mfano wa kuiga ni kuwa ushuri husaidia bajeti ya serikali kila mwaka”
.alisema Murekezi.

Iwapo waziri mkuu husema hayo, alitangaza kuwa hatujafika mwisho yaani tunaendelea na safari kwani asilimia kubwa ya bajeti misaada ya kigeni.

“Haya ni mambo wazi, nchi fulani kuchukua kodi ya wananchi na kusaidia nchi nyingine, haya hayafanywi bila sababu yaani ni faida ya nchi hiyo. Tunapaswa kujua kuwa kodi ni ngao muhimu mbele ya nchi za kimataifa, tunawaomba kufanya kwa bidii ili tutimize ahadi tuliotekeleza”
. Waziri mkuu aliongeza.

Kusherehekea siku ya walipakodi tarehe 22 Agosti 2016, Rwanda Revenue Authority (RRA) imewazawadia walipakodi bora MTN RwandaCell , Crystal Ventures Ltd , I & M Bank, na Cimerwa Ltd.
Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments