Kakwambia ana ‘mtu’ ? fanya hivi, acha papara

SIKU hizi watu wengi ni waoga sana na suala la mapenzi. Si kosa lao. Utapeli na uongo wa watu wengi umesababisha hali hiyo. Fikiria kwa makini mchango
ndugu Ramadhani Masenga.

Wanawake wengi wanapoitwa na wanaume basi hujikuta wakiamini ni lazima tu atongozwe. Huku pia kichwani akijua akikubali tu, basi atakuwa ameungana na kundi la wanawake wengi katika mahusiano na mwanaume huyo. Iko hivyo.
Watu wanapangwa kama foleni za madumu visimani. Uoga wa maradhi na mambo mengine umewatoka.

Ila hii si kwa wanaume wote. Wapo walio makini na wanaojali na kuheshimu kiuhalisia hisia za wengine katika kiwango stahiki. Lakini ni nani ajuaye kuwa fulani anaweza kuja kuwa bora katika maisha yake kwa kumwangalia ? Hakuna. Macho si rahisi kukujulisha kilicho katika nafsi ya mtu.

Hapa umakini na subira ya kina inahitajika kumjua nani anaweza kuwa nani katika maisha yako. Kutokana na hali hiyo, wanawake wengi wameamua kufanya kitu.
Sasa kila mwanamke unayemtongoza hata kama hana mchumba basi atakwambia anaye. Japo mbinu hii haiwasaidii sana, ila imeleta nafuu angalau. Wengi wao baada ya kuambiwa hivyo, hujikuta nafsi zao zikikata tamaa bila kujua wapo mtegoni.

Wapo wengine walio wageni katika mapenzi hivyo hawajui balaa lililowaandama wanawake wengi, kiasi cha kusingizia wana wachumba ilhali wakiwa hawana. Mwanamume wa aina hii akiambiwa tu ‘nina mchumba’, basi moyo humuuma na kuamini haikuwa riziki yake.

Mwanamke anaweza kukujibu namna hiyo kama umemuuliza kuhusu suala analohisi ni la ndani na sana. Kama vile nambari ya simu, kumpeleka matembezi au ukijidai kutaka kujuana naye zaidi katika hali ya ukaribu zaidi.

Unatakiwa utulize vizuri akili yako, huku ukiamini bado mchezo uko upande wako. Usioneshe hali ya kukwazika na maneno yake, badala yake unaweza kutoa tabasamu fulani la kuonesha kumwelewa. ila chunga sana tabasamu hilo lisitoe tafsiri ya kufurahia maneno yake.

Onesha thamani yako kwa kuongea naye taratibu kwa hatua huku pia ukimpa naye nafasi ya kuchangia chochote anachoona kinafaa. Wanawake wanapenda sana mwanamume mwenye kujiamini.

Kwanza, kutaka kuonesha thamani yake na hadhi. Kwamba yeye ni msichana mwenye mvuto na kuna mtu kamuwahi tayari. Lakini pili, huwa anahitaji kuona vile utakavyochukulia jambo lenyewe. Kazi ni kwako.

Hapa unatakiwa kuwa katika hali ya utulivu na amani na kuanza kupanga maneno yako vizuri. Acha kuongea kama umekariri, kwani atazidi kukupa tabu kwa kuamini muda si mrefu ‘mashairi’ yako yataisha.

Pia kumbuka mpaka kaamua kukusikiliza basi jua kakuheshimu na amevutiwa na wewe hata kwa kiwango kidogo, maana si kila mwanamume anayemsimamisha mwanamke husimama. Wapo wengi aliwakatalia kusimama. Kwako hiyo ni heshima, itumie vizuri.

Ongea naye kwa kujiamini huku ukijua kama kuharibu ama kujenga huo muda ndio wake. Epuka kulazimisha mambo, akitaka muda wa kukufikiria mwachie. Kwa leo niishie hapa.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments