Miaka 38 inapita , rais wa kwanza wa Kenya Jomo Kenyatta alitangazwa kufariki dunia

Mzee Jomo Kenyatta alikuwa kiongozi wa Kenya kutoka uhuru mwaka 1963 hadi kifo chake mwaka 1978, yeye aliwahi kwanza kama Waziri Mkuu kati ya 1963 na 1964 na kisha kama Rais kutoka 1964 kwa 1978. Yeye huchukuliwa kama baba mwanzilishi wa taifa la Kenya.

Kenyatta alikuwa mwenye elumu ya juu na mwandishi wa vitabu kadhaa kama Facing Mount Kenya kilichohusu ukombozi na historia ya Wagĩkũyũ. Alikuwa pia mwanzilishi na mhariri wa gazeti la kwanza kwa lugha ya Gĩkũyũ ambalo liliitwa Mũigũithania.

Kutokana na kuhusishwa na harakati za vita vya msituni vya kundi la Mau Mau alihukumiwa miaka saba jela mwaka1952. Pia anakumbukwa kama Pan- Africanist ambao walipambana na kung’ang’ania uhuru wa waafrika wote kwa ujumla.
Jomo Kenyatta alizaliwa 1893 na alifariki mjini Mombasa tarehe 18 Agosti 1978 na kuzikwa jijini Nairobi kwenye jengo la bunge.

Jina lake halisi lilukuwa Johnstone Kamau wa Ngengi. Alipewa jina la utani ambalo ni Mkuki wa Moto (Burning Spear). Jina la Kenyatta lilitokana na mkanda aliopenda kuuvaa ambao ulitengenezwa kwa shanga. Wagĩkũyũ wanauita kenyaata.

Aliwaoa wake wanne ambao ni Grace Wahu (m. 1919) Edna Clarke (1942–1946) Grace Wanjiku (d.1950). Mama Ngina (1951–1978) ambaye alikuja kuwa mke wa rais wa kwanza na ambaye ndiye mama yake Uhuru Kenyatta, rais wa sasa.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments