Afrika ya Kati : Rais Faustin Archange Touadera awapongeza majeshi ya Rwanda

Rais Faustin Archange Touadera amepongeza vikosi vya kulinda amani kwa mchango wao katika maendeleo ya nchi yake.

Siku ya mti ilisherehekewa tarehe 20 Agosti 2016 katika mji mkuu Banguiambapo idadi kubwa ya wakazi wa mji Bangui ilijiunga na wanajeshi wa Rwanda wa kulinda amani chini Afrika ya Kati (MINUSCA), kupanda miti katika GBAZABANGUI hifadhi ya msitu.

Katika hotuba yake, baada ya kupanda mti rais Touadera aliwashukuru wakazi wa Bangui kwa kushiriki katika tukio hili. Pia aliwashukuru wanajeshi wa RDF amabo hulinda amani kwa dhamira yao na utayari wa kuchangia katika maendeleo ya Jamuhuri wa Afrika ya Kati (CAR).

"Nashukuru pia vikosi vya kulinda amani vilivyotoka nchini Rwanda kwani tukio hili ni aina ya utayariwa kuchangia katika maendeleo ya nchi yetu", alisema Rais Touadera.

Rwanbatt3 ni miongoni mwa askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa walioko nchini Afrika ya Kati (CAR) kwa ujumbe wa kulinda amani. Baadhi ya majukumu ya Rwanbatt3 ni pamoja na kutoa usalama kwa Mheshimiwa Rais wa Central Africa Republic (CAR), ofisi ya rais na ikulu ya rais. Wao pia kutoa usalama kwa mitambo muhimu katika jiji la Bangui.


Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments