Ubalozi wa Rwanda nchini Congo Brazaville wazinduliwa rasmi

Mgemi rasmi waziri wa mambo ya kigeni nchini Rwanda Bi. Louise Mushikiwabo

Leo jumamosi tarehe 20 Agosti 2016 nchini Congo Brazzaville kulizinduliwa rasmi ubalozi wa rwanda nchini humo.

Mwaka 2011, kulisainiwa mkataba wa ushirikiano katika ngazi mbalimbali ikiwemo usafirishaji wa anga, nishati, utalii, usalama, teknolojia nk.

Wakati wa uzinduzi rasmi wa ubalozi wa Rwanda nchini Congo Brazaville, waziri wa mambo ya kigeni alisema “Uzinduzi wa ubalozi ni matunda ya bidii na nguvu za marais wa nchi zote. Tangu tuliposaidi mkataba wa ushirikiano 2011, umoja na ushikamano uliongezeka katika njia ya kidiplomasia, hii ni njia ya maendeleo kama waafrika kama lengo la viongozi wetu”.

Waziri Mushikwabo alieleza kuwa nchi hizi mbili ziliunda kundi la wataalam watakaochunguza ingawa mkataba wa uchumi umeimalika na kufanya mkutano mjini mwanzoni mwa mwaka 2017. Aliwashawishi wafanyabiashara binafsi kutumia bahati hii wanayoipewa ya kufanya uwekezaji kati ya nchi hizi.

Dkt Habyarimna Jean Baptiste aliteuliwa kama balozi wa rwanda nchini Congo Brazaville Agosti 2015 lakini alianza majumuku yake bila kuzinduzi rasmi. Miezi 3 iliyopita ndipo kulizinduliwa ubalozi wa Congo Brazzaville mjiji Kigali.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments