Rusizi : Kabla ya kifo cha washukiwa wa ugaidi, walimulaana na kumuvunjia heshima Imamu

Sheikh Nzabonimpa Swalleh, Imamu wa mskiti wa Bugarama /photo N Niyibizi/Umuseke

Jana tarehe 19 Agosti 2016 ndipo kulienea habari za kifo cha watu 3 katika kata ya Bugarama wilayani Rusizi ambao walipigwa risasi na kuuawa na jeshi la polisi wakati waripojaribu kutoroka, watu hao waliotuhumiwa vitendo vya ugaidi.

Katika kipindi chA kuwapa moyo wananchi, Imamu wa msikiti wa Bugarama Sheikh Nzabonimpa Swaleh alisema “Tafadhali ! Mtoke ndani ya nyumba tuongee ili tujue tatizo lenu lakini wote walinijibu kwa sauti moja na maneno ya kiarabu wakisema kuwa laana za Mungu zinifikie. Tumewafukuza msikiti kwa sababu ya kufundisha imani ya msimamo mkali”.

Kiongozi mkuu wa jeshi la polisi mkoani Magharibi ACP Mutezintare Bertin alisema “Waliojaribu kuharibu usalama wetu ndio waliopata hasara kubwa. Yeyote mwenye fikra za kuharibu usalama atapata hasara kabla ya kuharibu usalama wetu”.

Jeshi la Polisi nchini Rwanda limetangaza kuwa Eric Mbarushimana, Hassan Nkwaya wanasemekana kuwa na asili ya wilaya ya Kamonyi na Kicukiro pamoja na Moussa Bugingo ambaye alifariki dunia wakati alipofikishwa hospitalini. Shafi Cyiza ambaye hujeruhiwa analazwa hospitali na kutibiwa kabla ya kufikishwa mahakamani.

Latiffah Morina na Aboubakar Ngabonziza wenye asili wilayani Kamonyi hufungiwa kwenye kituo cha polisi cha Bugarama wakati upererezi unapoendelea.

Wananchi wakihudhuria mkutano

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments