Rais Pombe Magufuli amuomba msaada Dkt Donald Kaberuka

Dkt Donald Kaberuka aliyekuwa mkuu wa Benki ya Afrika ya Maendeleo (BAD), jana tarehe 19 Agosti 2016 aliongea na rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Joseph Magufuli jijini Dar es Salaam kuhusu uchumi wa taifa hilo.

Rais Magufuli alimshukuru Kaberuka bidii yake na uangalifu alivyoonyesha wakati alipoongoza benki hii na kumuomba kuendelea kuishauri Tanzania kiuchumi.

Kama alivyotanga rais Magufuli alisema “Nchi yetu itaendelea kushirikiana na wewe, tunatumaini kuwa bado una moyo wa kutushauri katika mipango yetu ya kimaendeleo jinsi tutakanufaika na kuzalisha rasilimali, ardhi kubwa, mifugo kama ng’ombe, ziwa na bahari pamoja na hifadhi”.

Dkt Kaberuka alimshukuru rais Magufuli kwa mikakati aliyotekeleza ili aendeleze Tanzania ikiwemo kupiga marufuku rushwa, ukusanyaji wa ushuru, mapato na kodi na kulinda rasilimali ya nchi. Hapo ndipo aliposema kuwa bila shaka Tanzania itajiendeleza.

Kaberuka (mtaalum katika uchumi) mwenye umri wa miaka 61 aliongoza Benki ya Afrika tangu 2005 hadi 2015, kwa usasa habari zinazoenea katika masikio ya wengi ni kuwa ni mwenye bahati ya kushindia kiti cha rais wa tume ya Umoja wa Afrika (AU) ingakuwa hajasema hata kitu kimoja kuhusu maombi hayo.

Tume hii inamtamani mtu ambaye ataisaidi kupunguza mikopo ya mataifa ya kigeni hadi 75 % kwa kutafuta jinsi afrika yaweza kujiendeleza bila kutemegea fimbo ya mbali.

Kaberuka (kushoto) akiwa pamoja na Rais Magufuli (kulia)

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments