Kigali : Watu kumi washikiliwa na jeshi la polisi wakibeba pembe za ndovu

Jeshi la polisi nchini Rwanda limewakamata watu 10 wanaohusika katika biashara za pembe la ndovu, walitiwa nguvuni wakielekea barani ulaya, baadhi ya watu hao kulikuwemo watu ambao si wanyarwanda.

Makamu msemaji wa jeshi la polisi nchini Rwanda, Chief Superintendent of Police (CSP) Lynder Nkuranga alisema ”Baadhi ya washtakiwa kushiriki katika biashara za pembe la ndovu kulikuwemo watu 4 kutoka Gunea na wanyarwanda sita, walikuwa na kilo 80 za pembe la ndovu, walikuwa na lengo la kuenda barani Asia”.

Kuna habari ambazo husemwa kumba pembe hizo zilitoka Tanzania ingawa washitakiwa husema kuwa zilitoka nchini ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (RDC).

”Bado tunaendelea na upererezi ili tujue habari kamili kuhusu biashara za magendo na kutia nguvuni wahusika wengine ili wapelekwe mahakamani. Rwanda haiwezi kuvumilia biashara za magendo”. Nkuranga aliongeza.

Mwaka huu mwezi Aprili Mahakama ya rwanda yamewahukumu watu 4 kutoka Gunea na myarwanda mmoja kifungo cha miaka sita ambao walihusika katika biashara za pembe la ndovu.

Nkuranga alisema “Lengo letu ni kulinda mazingira na wanyama, majukumu yetu ni kulinda ndovu duniani kote na wanyama wote kwa ujumla, jeshi la polisi limeamua kutetea sheria husika kwani linashirikiana na mataifa yote kupiga marufuku uhalifu ulengao mipaka”

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments