Rusizi : Washukiwa wa ugaidi wa tatu wapigwa risasi na kuuawa

Watu watatu (3) ambao wanasadikiwa kuwa watuhumiwa kushiriki na makundi mbalimbali ya kigaidi yenye msimamo mkali waliuawa na jeshi la polisi la Rwanda wakati walipojaribu kukimbia na kutoroka.

Tukio hilo linasemekana kutokea Ijumaa hii ya 19 Agosti 2016 katika Kata ya Bugarama kijiji cha Nyange saa kumi na moja alfajiri.

Habari hii imethibitishwa na afisa mkuu wa jeshi la Polisi wilayani Rusizi SP Sano Nkeramugaba “Ilikuwa idadi ya watu sita wanaume 5 na mwanamke mmoja ambao walikuja hapa Bugrarama kufundisha imani inayoendani na msimamo mkali wa ugaidi ndipo jeshi la polisi lilipata habari kamili kuhusu watu hawo na kuenda kuwatia nguvuni. Watuhumiwa walikuja wilayani Rusizi wiki iliyopita.” Alisema SP Nkeramugaba.

Jeshi la polisi liliwapiga risasi watatu katiyao wakafariki dunia wakati walipojaribu kutoroka hapo ndipo mwingine alipojeruhiwa. Wengine wawili wariobaki ndani ya nyumba walitiwanguvuni na wanashikiliwa na jeshi la polisi ikiwemo yule mwanamke mmoja.

Watuhumiwa waliobaki wote wanakubari kuwa ni washiriki wa kundi la kigaidi na wanafuata imani na sheria za kigaidi.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments