Kigali : Ujenzi wa barabari hizi utapunguza msongamano mkubwa wa magari

Uongozi wa mji Kigali umetangaza kuwa ujenzi wa barabara ndogo zitakazosaidia barabara kubwa kwenye maeneo ya Kimihurura utawekwa mwishoni hivi karibuni.

Kunadhaiwa kuwa ujenzi wa barabara hizo utamalizika kujengwa mwishoni mwa mwezi Agosti. Siku hizi, kunajengwa barabara ya kilometa 7 kwenye sekta ya Kimihurura, barabara hii iko kwenye mpango wa barabara za kilometa 105 zitakazosaidia barabara kubwa katika maeneo mbalimbali mjini Kigali kwa lengo la kupunguza msongamao mkubwa wa magari.

Kiongozi wa masula ya miundo mbinu mjini Ahimbisibwe Reuben alisema “Mpango wetu ni kujenga kilometa 20 katika maeneo mbalimbali kwani wanainchi wanasubiri barabari hizo kwa hamu”.

Ujenzi wa barabara kwenye sekta kama Muhima, Kiyovu, Kabuga, Kimironko, Gisozi, Kimisange, Kibagabaga, Nyamirambo, Kagarama pamoja na Niboye utafuata baadaye.

“Tunawaomba wananchi kulinda barabari hizi kwani ni maendeleo yao, tunawashawishi kutosambaza uchafu ndani ya barabari, kusafisha njia zinazoenda nyumbani kwao, kupanda maua ndani ya uzio". Aliongeza.

Mwanzoni mwa ujenzi wa brabara hizi kulidhaiwa kuwa watatumia mawe lakini walipanga kujenza barabara za lami baada ya uhaba wa mawe.

Uhaba wa mawe ulisababisha kunungunika kwa wananchi baada ya kuzidiwa na vumbi, lakini kwa sasa uamuzi uliochukuliwa ni kujenga barabara za lami.
Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments