Kigali : Mtuhumiwa wa ugaidi apigwa risasi na kuuawa Jeshi la polisi

Jeshi la polisi nchini Rwanda limempiga risasi na kumuua mtu mmoja aliyetambuliwa kuwa ni Mbonigaba Channy ambaye alikuwa anatuhumiwa kuwa gaidi usiku wa kuamkia Alhamisi hii.

Katika tangazo la Jeshi la Polisi Jijini Kigali Rwanda mapema tarehe 18 Agosti 2016, mtu mmoja aliyekuwa anashukiwa ugaidi alijibizana risasi na polisi katika maeneo ya Nyarutarama wakati polisi walipomtaka mtuhumiwa huyo kwa jina la Mbonigaba Channy kujisalimisha baada ya kutambua hila zake za kigaidi lakini badala yake mtuhumiwa aliwafyatulia risasi polisi na kuendelea kutishia usalama wa eneo hilo.

Mbonigaba aliendelea kujifungia ndani ya nyumba moja ya kifahari wakatimwingine akitoka na kufyatua risasi ambazo ziimjeruhi afisa mmoja wa police. Polisi hao walidhibiti hari hiyo na baadae kufanikiwa kumchapa risasi mtuhumiwa anayeripotiwa kufariki katika eneo la tukio. Kwa usasa polisi aliyejeruhiwa alipelekwa kwenye hospitali la mfalme Faisal mjini Kigali.

Marehemu Mbonigaba anasemekana kuwa na asili ya wilaya ya Rubavu inayopakana nan chi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) upande wa mashariki Jeshi la polisi nchini Rwanda limewahakikishia wakazi wa eneo la Nyarutarama na maeneo mengine Jijini Kigali nan chi nzima kwa ujumla kuwa usalama umeimarika tena na hari sasa ni shwari.

Si mara ya kwanza kutokea habari zinazohusiana na ugaidi Nchini Rwanda hasa kwakuwa Januari mwaka huu jeshi la polisi lilimpiga risasi mtuhumiwa mwingine wa kigaidi aliyeitwa Muhammad Mugemangango ambaye wakati huo alikuwa katika mikono ya sharia ambapo alikuwa amefungiwa kwa muda katika kituo cha police cha Kanombe Jijini Kigali kabla ya kupelekwa mahakamani.

Mtuhumiwa huyo Mohammad alipigwa risasi pia akitaka kutoroka kutoka katika gari la police ambalo lilikuwa linamhamisha kutoka sehemu moja hadi nyingine. Ikiwa amepatikana na hatia, mshiriki wa ugaidi huhukumiwa na sharia katika katiba ya Rwanda kwa kifungo kati ya miaka 15 hadi 25 kama inavyonukuliwa na ibara ya 497 hadi ibara ya 528.

Imeandikwa na Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments