Kocha Jonny MCKinstry aonyeshwa mlango

Kocha mkuu wa timu ya taifa (Amavubi) anafukuzwa kazini baada ya mporomoko mkubwa wa timu ya taifa kwenye orodha ya Shirikisho la Kimataifa la Chama cha Soka (FIFA) ambayo hutangazwa kila mwezi.

Habari za kuamininika zinazofikia kwenye Makuruki.rw zinasema kuwa meneja wa timu ya taifa nchini Rwanda Jonny MCKinstry amefutwa kazini. Habari hizi zinakuja baada ya magazeti mengi nchini yalisambaza na kutangaza kuwa kocha huyo atafukuzwa kazini leo hii Alhamisi.

McKinstry mwenye umri wa miaka 30 alifika nchini Rwanda mwaka 2015 mwezi Mechi wakati alichukua nafasi Stephane Constantine raia wa Uingereza ambaye alichukua majukumu kama kocha wa timu ya India.

Wakati Jonny MCKinstry alipochukua majukumu haya, timu ya taifa ilikuwa kwenye nafasi ya 68 kwenye orodha ya FIFA na kuahidi wanyarwanda kuwa atafikisha timu hii kwenye nafasi ya 50 lakini jambo la kusikitika na kushangaza ni kuwa Rwanda iko kwenye nafasi ya 121.

Katika siku silizopika MCKinstry alitangaza kuwa hajui habari kuhusu kufutwa kazini kwani anajianda mechi ya timu ya taifa pamoja na Ghana ambayo itachezwa mwishoni mwa wiki hii.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments