Aliyeokolewa kutoka Boko Haram asema anamkosa baba wa mtoto

Msichana mmoja raia wa Nigeria ambaye aliokolewa kutoka mikononi mwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu wa Boko Haram, amesema anamkosa sana mpiganaji wa kundi hilo ambaye ni baba wa mtoto wake.

Amina Ali ni mmoja wa wasichana mia mbili wa shule ya Chibok waliotekwa nyara miaka miwili iliyopita. Amesema kile anachotaka sasa ni kwenda nyumbani.
Yeye pamoja na mtoto wake wamekuwa wakizuiliwa katika mjini Abuja, katika kile serikali inasema ni mpango wa kumwezesha kutengamana na watu tena.

Kinachomhuzuniza ni kuwa serikali ilimtenganisha na mmewe Mohammed Hayatu na kumpeleka mahali yeye hajui lakini mmewe anafungiwa katika jela ya majeshi ya serikali ya Nigeria wakati upererzi unaendelea kufanywa.

“Sifurahii kuwa pekee yangu kwani tumetenganishwa na wakati natamani ajue kuwa bado namuaza siwezi kumsahau”. Amina alisema.

Amina Ali alipatikana katika msitu mmoja mapema mwaka huu akiwa na mtoto wake na mtu mmoja ambaye alisema ni mumuwe ambaye ni mpiganaji wa kundi hilo la Boko Haram.

Amina na mmewe Mohammed Hayatu

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments