Askari Polisi wa Rwanda wasifiwa kwa kazi kubwa nchini Sudan Kusini

Askari Polisi 240 wakiwemo wanawake 47 ambao huunda kundi la FPU wanaolinda amani nchini Sudani Kusini (UNIMISS), tarehe 15 Ogasti walisifiwa kwa kazi kubwa waliyoifanya nchini humo.

Katika hotuba yake Kamishna mkuu wa Polisi katika UNMISS CP Munyambo ambaye alikuwa mgeni rasmi alisema “Tunawashukuru kwa kazi yenu mliyoifanya mlionyesha adabu, mlifanya kwa bidii katika mwaka wote mliotumikia jamii hii, mlifanya iwezekanavyo ili nchi hii iwe na amani ya kudumu na kumaliza vita vilivyoua wananchi wengi wa Sudani Kusini na wengine kuachwa bila makao, tunawashukuru sana kwa ujenzi huu”.

Kiongozi wa ofisi ya Upper Nile katika Malakal, Hastings Amurani alisema “Hakuna kitu cha kushangaza kuwa askari polisi wa Rwanda wamesimama imara na kupeperusha bendera la nchi (Rwanda) bila kusahau bendera la Umoja wa Mataifa (UN) katika Sudani Kusini, bidii na uvumilivu wao ulionekana kwenye ngazi zote isipokuwa kuweka maisha yao hatarini, tunawashukuru kuwa hamkuonyesha uzembe. Vilituonyesha kuwa tunapaswa kushirikiana kati yetu kwani nyie ni mfano wa kuigwa bila shaka tutafuta nyao zenu”.

Kiongozi wa askari polisi wa Rwanda ACP Rutikanga aliwashukuru waliopewa na kuvishwa nakshi kwa adabu imara, ushirikiano kama nguvu walivyonyesha kama kitambulisho.
Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments