Wimbo Indoro wa Charly na Nina wavunja rikodi

Wimbo indoro wa Charly na Nina unachukuwa nafasi kubwa kwenye orodha ya nyimbo za wasanii kutoka jamii ya wanyanrwanda ambao umetanzamwa na idadi ya watu milioni kwenye mtandao wa Youtube.

Kundi la mabinti wawili Charly na Nina limeshika kamba katika sekta ya mziki hapa nchini kwa muda mfupi, haya ni matokeo baada ya kushirikiana na msanii kutoka Burundi Big Fizo katika wimbo wao Indoro.

Wimbo huo uliwasaidia kuingia na kufungua milango ya nyumba ya mziki nchini Rwanda kwani walianza kukaribishwa kwenye tamasha mbalimbali hasa hasa nje ya nchi ikiwemo DRC (Goma) na Uganda. Kwa sasa kundi hili linapigania nafasi nyingi katika Salax Awards.

Watu zaidi milioni walitazama wimbo huu (Indoro) kutoka tarehe 30 Novemba 2015 hadi leo hii, inaama kuwa ni muda mfupi usiozidi mwaka, watu 2000 waliupenda, watu 220 walionyesha kuwa hawavutiwi na wimbo huo wakati ambapo watu 160 walionyesha hisia zao wakiandika maneno ya kusifu wimbo huo. Kundi la mziki wa nyimbo za injili nchini Burundi liliimba wimbo wakitumia beat ya wimbo indoro.

Mwanzoni mwa mwaka huu 2016 Meneja wa kundi hili (Charly na Nina) Muyoboke Alex alitangaza kuwa watafanya remix na msanii machachari kutoka Tanzania Ali Kiba lakini hakuna kitu kilichofanywa kwa sasa.

Kuna nyimbo zilizotazamwa mara milioni kama Nka Paradizo, Burinde Bucya za Meddy akishirikiana Pricilla.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments