Gari la UNHCR lililobeba bangi lafanya ajali

Gari la Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi nchini Rwanda (UNHCR) Toyota Land Cruiser lilifanya ajali kwa sababu ya mwendo kasi na kukuta kilo 86 za bangi, dereva wa gali hilo alitoloka moja kwa moja.

Msemaji wa jeshi la polisi mkoani magharibi Chief Inspector of Police (CIP) Theobard Kanamugire alisema kuwa ajali hiyo ilitokea kwenye kijiji cha Kadashya kiini cha Kanazi, sekta ya Ruharambuga wilayani Nyamasheke tarehe 16 saa tano za jioni.

Alisema "Dereva alikuwa anaongoza mtokaa hiyo kwa kasi ya ziada kisha motokaa iliporomoka . walinda amani ambao walikuweko kandokando ya hapo ndio walikuja kutoa usaidizi, kighafla walishangazwa kuona bangi kwenye gari hiyo. Nambari ya usajili ya motokaa hiyo ni IT 904 RD , wakati huo huo polisi ilifika na kupeleka bangi kwenye kituo cha polisi cha Ruharambuga”.

CIP Kanamugire alisema kuwa wanamtafuta dereva huyo wakati upererezi unaoendelea ili kumshika nguvuni mshiriki yeyote anayehusika katika biashara za bangi.

“Tunaomba Asasi zisizokuwa za Serikali non-governmental organization (NGO) kuwapa madereva kazi ambao ni waaminifu wasioweza kufanya kinyume na sheria za serikali na jamii . tunashukuru wananchi kwa ushiriki wao wa kutoa habari kwa muda mwafaka ili kuwashika washiriki wa mipango ya kikatili” CIP Kanamugire aliongeza.

Aliwakumbusha pia kuwa bangi ni mojawapo ya madawa ya kilevya na ni adui wa amani na mwanzo wa matendo ya kikatili yanayoleta vuruga na ukosefu wa usalama katika jamii.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments