Washauriwa kabla ya kuanza majukumu

Kiongozi mkuu wa polisi nchini Rwanda IGP Emmanuel K. Gasana aliwaomba maafisa wa polisi 405 waliopandishwa katika cheo cha Assistant Inspector of Police (AIP) (nyota moja ) kuleta mapinduzi katika majukumu yao, kufanya kwa bidii kulingana na masomo waliyopewa. Walipewa maonyo hayo katika makao makuu ya polisi nchini Rwanda katika maeneo ya Kacyiru mjini Kigali.

IGP Gasana alisema ”Mnaombwa kufanya kwa bidii kama ngao yenu, wanyarwanda wanangojea mavuno ya kutosha, lakini kufikia kwenye mavuno hayo mnaombwa kusikia na kuweka matendoni yale masomo mliyosomeshwa kwa mwenendo fasaha".

Wakati wa kupewa mashauri hayo kabla ya kuanza majukumu yao, viongozi tofauti kutoka ngazi zote za polisi walihudhuria.

IGP Gasana aliongeza “Mnapaswa kutumia ujuzi mliopewa na kupambania kufikia kwenye lengo la polisi hasahasa kwa nchi yenu. Adabu iwe ngao yenu ya kilia siku hata na milele”.

Aliwakumbusha kupigana na kitu chochote kinachoweza kutia matope sura ya nchi na polisi kwa ujumla.

Adabu kama ngao

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments