Sina hofu ya kurudi nchini ya kuzaliwa “Kidum Kibido”

Kidum alisema kwamba kuna watu wasiojulikana wanaojiita majina ya wanasiasa ambao wanampangia mipanga ya kikatili kwa kumuambia kuwa watamuua wakati atakapoenda kufanyia tamasha nchini Burundi mwezi Septemba.

Kwa kuwajibu, aliwaambia kuwa hana hofu na hawezi kusimamisha mpango wake bila shaka waendelee mpango wao wa unyama, aliandika kupitia facebook yake tarehere 15 Agosti 2016.

Kidum alisema “Wewe unayepanga kuniua mie Kibido Kibuganizo kisha ukanitega mitego kwenye facebook na kujiita majini ya wapinzani wa serikali yetu, siwezi kuhofia hayo, unataka niwe na hofu ya kuja nchini mwangu. Nitafika Bujumbura tarehe 1 Septemba 2016. Panga jinsi utakavyoniua wakati huo. Wakati utakapotimiza mipango yako kama ulivyopanga ndiyo njia ya kunisaidia kuaga dunia katika nchi ya babu”.

“Jipange sawasawa kwani njia na mbinu zote nimezitambua, mie si mshiriki wa vyama vya upinzani, hakuna kitu kingine ambacho nategemea kama manufaa yangu, isipokuwa mziki siwezi kusimamisha mziki hivi karibuni” Kidum aliongeza.
Alimaliza ujumbe huu kwa kusema “Mungu ni mkubwa, nakuja bila shaka”.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments