Kiir ataka bunge kuamua kuhusu wanajeshi wa UN

Habari kutoka VOA inasema kwamba rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, analiachia bunge la nchi hiyo kuamua iwapo litakubali au kukataa azimio lililopitishwa na baraza la usalama la umoja wa Mataifa, kutaka kupeleka wanajeshi wa kigeni 4,000 nchini humo.

Baraza hilo liliidhinisha kupelekwa kwa wanajeshi Zaidi mnamo siku ya Ijumaa wiki iliyopita.

Rasimu hiyo ambayo iliwasilishwa na Marekani, pia inapendekeza vikwazo vya silaha, endapo Sudan Kusini itakataa kupelekwa kwa wanajeshi hao.
Vikosi hivyo vitapelekwa mjini Juba, na vimepewa idhini ya kutumia kila mbinu kuhakikisha kwamba azimio hilo limefuatwa kikamilifu.

Martin Hubert IKURAMUTSE

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments