Rwanda yateketeza pembe za ndovu.

Mwezi mei, moshi mweusi ulitanda kwenye anga za mbuga ya kitaifa ya wanyama Nairobi baada ya Rais Uhuru Kenyatta kuchoma moto toni 105 za pembe za ndovu.

Kama Kenya ilivyofanya siku za nyuma, leo hii ya tarehe 12, Agosti, 2016 bodi ya maendeleo nchini Rwanda RDB yateketeza kilo 150 za pembe za ndovu alipokonywa majangili pamoja na vifaa vilivyotumiwa kwa kuua hao wanyama na kuchimba migodi kinyume na sheria.

Hii ni hatua iliyofanyika wilayani Nyamasheke, Magharibi mwa Rwanda.

Rugerinyange Louis, mkuu wa mbuga ya wanyama ya nyungwe iliyoko magharibi mwa Rwanda alisema kwamba kuchoma moto pembe si hatua ya kujivunia, kitu muhimu ni kuwa na ndovu hai.

Belise Kariza, msimazi wa utalii katika RDB aliwaomba raia walioshuhudia hii hatua na wanyarwanda kwa ujumla kuachana na sifa ya ujangili. Kwani kujangili ni kuharibu uchumi wa nchi ya kesho.

Pembe ambazo ziliteketezwa ni zenye thamani ya 300.000 dola za kiamrekani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments