Rwanda, Ujerumani kukubaliana milioni 48 dola za kimarekani

Mueller (kushoto) akiwa na mwanafunzi wa chuo cha ufundi,IPRC Kigali, na waziri wa elimu Dkt Papias Musafiri Malimba
Rwanda na Ujerumani wako katika mazungumzo ya mwisho ili kufikia dau la milioni 84$ dola za kimarekani , theluthi moja ya pesa zinazotarajiwa kutumiwa kwa kuimarisha utoaji wa elimu ufundi TVET.

Hii taarifa ametangazwa jana kufuatia mazungumzo ya kipekee kati ya waziri wa fedha na mipango ya uchumi Bw. Claver Gatete na waziri wa ushirikiano kiuchumi na maendeleaob wa Ujerumani, Dkt Gerd Mueller.

Akiongea na wanahabari mjini Kigali, Gerd Mueller alisema hii ni kwa lengo la kusaidia uwekezaji binafsi.

‘’tumekuwa kujadili milioni 84 $ ifikapo mwaka wa 2017, huu utakuwa msaada muhimu kwa miaka ijayo kwa ajili ya miradi maalum. naamni kuwa tutafanikiwa kwa kuvutia makampuni mengi ya Ujerumani kama tulivyokubaliana na Claver Gatete .’’ Waziri wa Ujerumani alisema.

Mueller aliongeza kuwa anashukuru serikali ya Rwanda kwa nguvu wanazotumia kwa kuimarisha uchumi wa nchi.

Na yeye aliahidi kuwa nchi yake itaendelea kutoa msaada.

‘’kutokana na uzoefu wake, Ujerumani inafamu jinsi ni vigumu kufikia mafanikio na maendeleo, wakati wewe ukianzia chini. Tutaendelea kusadia kazi ya serikali kwa lengo la kuimarisha utawala bora na utoaji wa elimu ya ufundi.’’
Mueller aliongeza.

Waziri Gatete alisema Ujerumani imekuwa kusaidia Rwanda kwa miaka mingi katika nyanja mbalimbali, hususan katika mashule ya TVET, kitu ambacho Gatete alisema kinaweza kuchochea maendeleo kwa watu wengi.

‘’masomo ya ufundi ni muhimu sana, sekta nzima ya viwanda inahitaji watu wenye ujuzi hii ndio maana ya masomo ya ufundi anahitajika sana kwa ajili ya uchumi wowote kukua.’ Gatete alisema.

Ruzuku inakuja baada ya miaka mitatu serikali mbili kufikia makubaliano matatu ya msaada thamani milioni 15 Rwf za kusaidia mashule ya TVET.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments