Rais Kagame na Kabila katika mkutano wa kuimarisha urafiki

Rais wa Rwanda Paul Kagame anatarajiwa kukutana na mwenzake Bw. Joseph Kabange Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Wilayani Rubavu, kasikazini mwa Rwanda karibu na mpaka.

Akitumia ukurasa wake wa Twitter, Bw. Julien Paluku, gavana wa Kivu kasikazini, alitangaza kwamba hawa marais wawili watakutana wilayani Rubavu nchini Rwanda hii ijumaa.

Kabila anamtembelea mwenzake Kagame baada ya kukutana mjini Goma katika mwaka wa 2009, hii ziara inafanyika kwa mara ya pili mfululizo baada ya ya Rais huyo wa Kongo kuhudhuria mkutano mkuu wa umoja wa Afrika uliofanyika mijini Kigali mwezi jana.

Licha ya Paluku kutangaza mkutano wa hawa marais wawili, yeye hakukutangaza ni nini ambacho watajadili katika huu mkutano wa kipekee.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments