KIGALI CAR FREE DAY kurudi tena.

Jumapili ifuatayo wanamji watashuka mitaani kwa kufanya mazoezi ya kuinua mwili kwa mwito uliotolewa na uongozi wa mji wa Kigali kwa ajili ya kuwahamasisha wanyarwanda kufanya spoti ili kujikingia maradhi kama mshituko wa moyo na nyinginezo.

Watu ambao wanaishi karibu na maeneo ya mji watakutana katika car free zone mjini saa moja za asubuhi na wengine wanaoishi karubu na maeneo ya Remera watakutana kwenye uwanja wa taifa Amahoro.

Wote watakutana katika Kimihurura kwenye makao makuu ya mamalaka ya mapato Rwanda ambako watachapa mazoezi ya kuinua misuli na kupimwa maradhi zisizoambukizwa kimakusudi.

Huu ni mwito uliotolewa na Mji wa Kigali kwa ajili ya kukumbusha wanyarwanda faida za kuchapa mazoezi na kuwahamasisha kujikingia maradhi zisizoambukizwa kama saratani, mshituko wa moyo, kisukari na nyinginezo.

Car Free day itakuwa kwa mara ya tatu kufanywa tangu kuanzishwa na mji wa Kigali.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments