Balozi wa Rwanda katika umoja wa mataifa afutwa kazini

Richard Eugne Gasana ambaye aliyekuwa balozi wa Rwanda katika umoja wa Mataifa amefutwa kazini kutokana na taarifa ilyotolewa na kikao dharura cha mawaziri kilichofanyika jana tarehe 10, agosti, 2016 katika Ikulu ambacho kulikuwa kuongozwa na Rais Paul Kagame.

Balozi Richard Eugene Gasana aliwakilisha Rwanda katika umoja wa mataifa tangu mwezi Aprili, mwaka wa 2013 ambako katika mwaka huo huo mpaka mwezi Aprili, 2014, Yeye aliongoza baraza la usalama la UN wakati Rwanda ilipokuwa mwanachama asiye kudumu wa baraza hilo.

Gasana ni mwenye umri wa miaka 20 katika shughuli za kisiasa, kwenye majukumu ya kisiasa, Gasana alikuwa balozi wa Rwanda katika nchi mbalimbali zikiwemo Ujerumani, Austria, Bulgaria, Jamhuri ya Czech, Urusi, Hongary, Poland, Romania na kadhalika.

Na Gasana alikuwa mfanyakazi katika ubalozi wa Rwanda katika Ujerumani,(1994-1995), na Uswisi(1996-1997.)

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments