Akamatwa kwa kupanda mnara wa makao makuu ya Trump Marekani

Polisi wakijitahidi kumuondoa
Mtu mmoja aliyejaribu kupanda jengo la Trump Tower lililopo jijini New York, ameondolewa na polisi katika jengo hilo baada ya kuchomwa na vioo vya jengo hilo lenye ghorofa 58 ambalo ni makao makuu ya kampeni za kumchagua Donald Trump.

Mpandaji alionekana amelewa
Trump anaishi kwenye chumba cha juu ya ghorofa hilo lakini kwa sasa anafanya kampeni zake nje ya mji.

Mpandaji alijivuta huku akiwa akionekana kuwa amelewa, akitaka kuingia ndani ya jengo hilo.

Umati wa watu ukishuhudia polisi wakimuondoa
Polisi waliofika eneo la tukio wamesema hawakuweza kutambua nini haswa lilikuwa lengo lake.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments