Waziri wa Ujerumani kutembelea Rwanda.

Waziri wa Ushirikiano kiuchumi na maendeleo nchini Ujerumani Dkt Gerd Mueller anasubiriwa mjini Kigali katika ziara ya siku mbili.

Ziarani yake ambayo itamalizika ijumaa, Gerd Mueller atazingatia mashule ya ufundi na utawala bora.

Akiwa pamoja na waziri wa elimu Dkt Papias Malimba Musafiri, Mueller anatarajiwa kutembelea chuo cha elimu ya ufundi mjini Kigali (IPRC Kigali) kwa mujibu wa taarifa.

Baadaye, waziri huyo kutoka Ujerumani atakutana na waziri wa Uchumi Bw. Claver Gatete kisha akutane na wandishi wa habari kabla ya kuzuru makumbusho ya mauaji ya kimbari dhidi ya watutsi ya Gisozi/mjini Kigali.

Mwezi Juni, Kwa ushirikiano kati ya serikali ya Rwanda na Jamhuri ya Ujerumani Mamlaka ya elimu ya ufundi WDA ilitangaza kuwa inajipanga kununua vifaa vya kisasa thamani ya billion 4,6 Rwf kwa ajili ya kuimarisha elimu ya ufundi katika mashule tano ya TVET.

Kabla ya kuzuru Rwanda, Waziri Mueller alikuwa nchini Senegal na Niger

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments