Mkuu wa zamani wa RSSB afutiliwa mashtaka

Aliyekuwa mkuu wa taasisi ya bima ya kijamii RSSB amefutiliwa mashtaka kama msemaji wa mahakama za Rwanda alivyothibitisha.

Angelique Kantengwa alikamatwa na kufungwa mwezi Septemba, mwaka wa 2014 akishtakiwa matumizi mabaya ya fedha za umma. Lakini mwezi Machi, 2015 mahakama makuu ya Nyarugenge aliamua kumfungua kwa muda kwa sababu ya hali mbaya ya maisha yake.

Angelique alikuwa akituhumiwa ubadhirifu wa zaidi ya bilioni 1.6 Rwf na kuzawadi raslimali za serikali kwa bure.

Bw. Itamwe Emmanuel, msemaji wa mahakama ya Rwanda alithibitisha kwamba Angelique amefutiliwa mashtaka.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments