Wasomali kumchagua Rais mwishoni mwa mwezi Oktoba

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud

Uchaguzi wa urais nchini Somalia umepangwa kufanyika tarehe 30 mwezi Oktoba mwaka huu, huku ule wa wabunge ukitarajiwa kufanyika kuanzia mwezi ujao.
Tangazo hili limetolewa na Tume ya Uchaguzi ya Somalia, inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa.

Kuelekea katika uchaguzi huo wa kwanza nchini humo baada ya muda mrefu wa ukosefu wa usalama nchini humo na Jumuiya ya Kimataifa inasema inatumai kuwa utarejesha amani nchini humo.

Wajumbe 14,000 kutoka kote nchini watakaokuwa wamechaguliwa na wazee wa koo mbalimbali nchini humo watakutana kumchagua rais, pamoja na wabunge 275.

Rais Hassan Sheikh Mohamoud ambaye muda wake unamalizika mwezi ujao ni miongoni mwa wanasiasa 10 wanaotarajiwa kuwania wadhifa huo.

Nchi ya Somalia imeendelea kukabiliana na changamoto za kiusalama kutoka na kuwepo kwa kundi la kigaidi la Al Shabab ambalo limesabisha vifo vya maelfu ya watu na wengine kukimbilia nchi jirani ya Kenya na Ethiopia kutafuta hifadhi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments