‘’Mimi si mungu, mimi ni kocha mwenye malengo’’ - Kocha wa timu ya kijeshi, Rwanda

Michezo ya Kijeshi (EAC military games) ilizunduliwa rasmi jana mjini Kigali katika uwanja wa taifa Amahoro, kwa mwanzo timu ya wanajeshi wa Rwanda ilicharazwa na wenzao wa Kenya goli moja kwa sahani.

Akizungumza na wandishi wa habari, Kanyankore Gilbert Yaounde ambaye ni mkufunzi wa timu hiyo na kocha wa APR FC alisema kwamba timu yake ilifungwa kwa sababu ya uzoefu mdogo lakini yeye anasema ingawa ya kubamizwa katika michezo ya kijeshi wao wanalenga kushinda na aliwahakikisha ushindi katika mechi zifuatazo mashabiki wa APR FC na timu iliyoshiriki hii michezo ya kijeshi.

‘’ mimi si mungu kwa kufanya maajabu lakini mimi ni kocha mwenye malengo ya ushindi, leo tumeshindwa lakini unaanza kidogo kidogo kwa kupata ushindi. Huwezi kula mazao ya kilimo bila kungoja siku na miezi , msikate tama, sisi tutashinda mechi zifuatazo na hata wakati wa msimu ujao wa ligi tutashinda.’’ Kanyankore alisema.

Kanyankore Gilbert Younde aliteuliwa kufunza APR FC mwezi uliopita na yeye anasema kwamba analenga kujenga timu imara ambayo inaweza kuzichapa timu za Rwanda, za ukanda na hata barani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments