EAC kuachana na wadhamini

James Fred Kidega
Wakati alipokuwa akizungumza na mkuu wa seneti ya rwanda, Bw. Fred James Kidega, spika wa bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki amesema kuwa nchi wanachama wa jumuiya hii wana nia ya kujitafutia bajeti asilimia 100 ya bajeti kwa ajili ya kuachana na wadhamini.

Kidega ameyasema hayo baada ya viongozi wa Afrika waliohudhuria mkutano mkuu wa umoja wa Afrika uliofanyika mjini Kigali kuamua kujengea AU bajeti bila kungoja misaada.

Na Kidega amesisitiza na jumuiya ya Afrika mashariki huu ni muda wa kuiga uamuzi huo wa hawa viongozi wa Afrika.

‘’tulikubaliana kujikimu kifedha pasipo kuombaomba watu wenye rehema.’’ Kidega amesema.

Yeye amesema kwamba anakubaliana na Bernard Makuza, mkuu ya seneti ya Rwanda, ambaye alibaini kwamba huu ni muda Afrika kuachana na misaada inayobeba faida kibinafsi.

Licha ya kusisitiza kujijengea bajeti, hawa viongozi hawakusema ni lini wao wataanza kutekeleza uamuzi.

Mwaka huu wa bajeti 2016/2017, EAC inatarajia kutumia $101,374,589 na pesa za wadhamini ni milioni 46.7 dola za kimarekani.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments