EALA kupeleleza sababu iliyofanya Burundi kufunga mpaka kati ya Rwanda

Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki husema kwamba Burundi huenda kudhibiwa kutokana na maamuzi ya nchi hiyo jirani na Rwanda ya kukata uhusiano wa kibiashara na harakati za magari ya abiria kati ya nchi hizo mbili.

Katika mazungumzo na mkuu wa seneti ya Rwanda (Bw. Bernard Makuza) ,
Mheshimiwa Daniel Fred Kidega ambaye ni spika wa bunge la jumuiya ya Afrika Mashariki alisema kwamba wao wanaenda kujadili tatizo hili lakini yeye alisisitiza kuwa jinsi ambavyo Burundi ilichukua maamuzi ni kinyume na sheria ya EAC ambaye inakubali harakati za raia, biashara katika kila nchi mwanachama wa EAC.

‘’tulisikia kwamba Burundi ilikata biashara na harakati za magari ya abiria kati ya Rwanda na Burundi. Katika nchi zote tano wanachama wa EAC ni lazima kukubali harakati za raia, huduma na biashara hii ndio maana sababu ya kujiunga.’’
Kidega alisema.

Mhe. Daniel Fred Kidega aliendelea kusema kwamba EALA inaenda kuchunguza kwa kina (kupitia tume yao) sababu iliyofanya Burundi kufunga mipaka na hatimaye wao watatoa mapendekezo ambayo huenda akawa adhabu kwa Burundi .

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments