Rais Kagame kutua Chad

Deby na Kagame
Hii jumatatu, Rais Paul Kagame wa Rwanda amefika mjini N’Djamena nchini Chad kwa kuhudhuria sherehe ya kumwapisha Rais Idriss Beby Itno ambaye alichaguliwa kuwa Rais wa nchi hiyo kwa muhula wa tano mfululizo.

Deby anaongoza Tchad tangu mwaka wa 1990 baada ya kumpindua Hussein Habre madarakani.

Katika sherehe hiyo ya Idriss kutawazwa rasmi, Rais Paul Kagame atakuwa pamoja na waziri wa ulinzi wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian, Rais wa Benin, Patrice Talon ; Rais wa Burkina faso, Rock Mark Kabore ; Rais Yoweli Kaguta Museveni wa Uganda ; Theodoro Obiang Nguema Mbasogo wa Equatorial Guinea, Mohammud Buhari wa Nigeria na wengineo.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments