Rais Erdogan azungumzia sheria ya kifo nchini Uturuki

Rais Erdogan amewaambia watu mjini Istanbul kuwa atapitisha sheria ya kifo kama italetwa tena na bunge la nchi hiyo.

Rais wa Uturuki Recep Tyyip Erdogan, amehutubia mkutano wa watu zaidi ya milioni moja baada ya jaribio la mapinduzi kushindwa mwezi uliopita.

viongozi wawili wa upinzani pamoja na mkuu wa majeshi waliungana katika mkutano huo kama ishara ya umoja.

Rais Erdogan amewaambia watu mjini Istanbul kuwa atapitisha sheria ya kifo kama italetwa tena na bunge la nchi hiyo.

Ujerumani imetoa onyo kwa Uturuki kama itapitisha sheria hiyo basi matumani ya yake ya kujiunga na umoja wa ulaya yataisha.

Rais Erdogan amesema nchi hiyo itaondokana na wafuasi wote wa mhubiri wa kimarekani Fethullah Gulen, mhubiri huyo amekataa kuhusika na jaribio la mapinduzi.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments