Idriss Déby atawazwa Jumatatu hii

Rais wa Chad Idriss Déby
Idriss Déby anatazamiwa kutawazwa Jumatatu hii, baada ya kushinda uchaguzi wa Aprili 5, uchaguzi ambo baadhi ya vyama vya upinzani vilipinga na kusema kwamba haviutambui.

Mjini Ndjamena, wakati ambapo marais na viongozi mbalimbali wanaendelea kuwasili kwa kuhudhuria katika sherehe ya kuapishwa kwa Rais Idriss Déby, upinzani ulifanya maandamano Jumapili hii Agosti 7katika miji mbalimbali nchini Chad.

Muungano wa vyama vya upinzani (FONAC), unaoendelea kupinga uchaguzi wa Aprili 5 uliandaa mfululizo wa mikusanyiko mwishoni mwa wiki hii. Mikusanyiko hiyo ilikua imepigwa marufuku na serikali, na ilisambaratishwa na vikosi vya usalama, kama Jumapili hii Agosti 7 mchana, lakini wakati huo matukio makubwa yalishuhudiwa. Mtu mmoja alipoteza maisha.

Kwa mujibu wa muungano wa vyama vya upinzani (FONAC),mtu mmoja alipoteza maisha katika makabiliano hayo. Taarifa ambayo imethibitishwa na vyanzo vya matabibuna chanzo cha polisi kwa RFI na kwa shirika la habari la AFP. Mtu mwengine yuko katika hali mbaya, baada ya kupigwa risasi tumboni.

Kwa mujibu wa FONAC, hali hii ilisababishwa na wanajeshi waliokuja kuunga mkono vikosi vya usalama. Watu kadhaa pia wamejeruhiwa baada ya kupigwa. Mtu mwingine alivunjika mguu wa kulia baada ya kugongwa na gari la vikosi vya usalama.

Waziri wa Usalama wa Raia anasema kuwa anachunguza tukio hilo. Hata hivyo siku ya jana hali ya wasiwasi ilishuhudiwa katika mji mkuu wa Chad.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments