Raia wa Rwimiyaga waonja mapato ya utalii

Wakiwa pamoja viongozi wa wizara ya elimu, wa jimbo la mashariki, wilaya Nyagatare na wa bodi ya maendeleo Rwanda walizindua jengo la shule ya msingi lilioko tarafa la Rwimiyaga, wilayani Nyagatare, jana tarehe 5, Julai, 2016 ambalo kujengwa na bodi ya maendeleo.

Hili jengo ni matokeo ya pendekezo la RBD lisemalo kuwa raia karibu na mbuga za wanyama au maeneo ya utalii hunufaika asilimia 5 kwenye mapato ya utalii.

Mwaka wa 2015/16 RBD ilikusanya milioni 318 dola za kimarekani, hii bodi inasema kwamba inatarajia kuwekeza pesa hizi katika miradi ya maji safi,umeme, mashule,
ili kurahisisha maisha ya raia ambao wanaishi karibu na mbuga za wanyama au maeneo ya utalii. Hii ndio sababu RDB ilichagua kuwajengea shule raia wa Gatebe/Rwimiyaga kwani ilikuwa muda mrefu watoto wao wakisomea chini ya miti.

Faustin Bumbakare ambaye ni mkurugenzi wa shule ya msingi ya Gatebe anasema kwamba mashule yalioko gatebe ni mashule ya watu ambayo anaharibika kila siku.

‘’ hapa gatebe tuna wanafunzi 1,914, jengo hili litatusaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi katika darasa moja, na saa tunafurahia umeme wa jua na one laptop per child.’’ Faustin alisema.

George Mupenzi ambaye ni meya wa wilaya ya Nyagatare amesema kwamba hii ni hatua ya kujivunia ambayo RBD inafanyia sekta ya elimu.

‘’hili ni jambo ambalo raia wanatambua ubora wake na wao wanafuraha sana.’’

Belise Kaliza ambaye ni msimamizi wa Utalii katika RDB alisema kwamba mapato ya utalii yanaingia katika bajeti ya serikali kwa kujenga vituo vya afya na vitendo vingine ambavyo serikali inahudumia raia.

Na kitu muhimu zaidi ni kwamba asilimia 5 ya mavuno ya utalii hutumika kwa kuwjengea raia miundombinu huishi karibu na mbuga za wanyama au maeneo ya utalii kwa ajili ya kuwaonesha raia sababu ya kuwahamasisha kulinda mbuga za wanyama.Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments