Mtu ambaye alijaribu kumuua Ronald Reagan kuachiliwa huru

Machi 30, 1981 katika nji wa Washington, John Hinckley alikamatwa kwa kujaribu kumuua Rais wa Marekani Ronald Reagan.

Mtu ambaye alijaribu kumuua Ronald Reagan Machi 1981 anatazamiwa kuachiliwa huru Ijumaa hii Agosti 5. John Hinckley aliwaruhiwa vibaya raisRonadl Reagan, msemaji wake, na askari polisi wawili, walipokuwa nje ya hoteli katika jiji la Washington.

Wakati wa kesi yake mwaka 1982, alikuwa Mahakam iliitangaza kwamba hana hatia kwa sababu za magonjwa ya akili. Uamuzi huo uliibua kashfa nyingi.

Baada ya uamuzi huo kusomwa, nia miaka karibu 35 sasa, 83% ya Wamarekani waliona kwamba haki haikutendeka. Ilikuwa vigumu kukubali kuwa John Hinckley hana hatia. Mtu huyu mwenye umri wa wa miaka 25 wakati huo,alidai kuwa alijaribu kumuua Rais ili kumfurahisha mwigizaji Jodie Foster.

Leo, baada ya miaka yote hiyo, wati mbalimbali wametoa hisia zao. Mtoto wa kwanza wa Ronald Reagan, Michael, anasema kama amerdhishwa na uamuzi huo kwa sababu baba yake alikuwa amemsamehe. Lakini dada yake, Patti Davis, amesema hatokua salama sasa.

John Hinckley apewa kifungo cha nyumbani

Masharti ya kufunguliwa kwa mfungwa huyo maarifu tayari yamechukuliwa kwa umakini. John Hinckley ataishi na mama yake mwenye umri wa miaka 90 na kila wiki atawajibika kumuhudumia kimatibabu. Hatoweza kujielekeza sehemu yoyote bila kutoa taarifa na anapaswa kujulishwa kama kutakuepo na mabadiliko ya ratiba yake.

Bw hinckley amepigwa marufuku ya kukutana na vyombo vya habari, na mtu yeyote mwenye uhusiano na jaribio la mauaji ya rais Reagan . Mashahidi wengi wanasema kwamba kifo cha Nancy Reagan, mwezi Machi, ni sababu kuu ya kuachiliwa kwake huru.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments