DCGP Mary Gahonzire, miongoni mwa maafisa wa polisi 300 waliostaafu

Sheikh Musa Fazil Harerimana ambaye Waziri wa usalama wa ndani ndie aliyeongoza tukio.
Jumla ya maafisa wa polisi 308 wamestaafu kutoka majukumu ya kipolisi, hawa maafisa ambao wakiwemo DCGP Mary Gahonzire ambaye alikuwa inspekta mkuu wa Polisi wa Rwanda miakani ya zamani na naibu mkuu wa taasisi ya huduma za kurekebisha.

Na wengine ni DCGP Stanley Nsabiaman, na makamishna wa polisi ambao ni Cyprien Gatete, makamishana msaidizi wa polisi wakiwemo Dk Wilson Rubanzana, Sam Karemera, Francis Nkwaya, Joseph Rudasingwa na Jimmy Hodari.

Kwa ujumla, polisi waliostafu ni makamishana nane, maafisa wandamizi 38, maafisa wadogo 62, non-commissioned police 156, polisi konstebow 44 na manaibu kamishna wakuu wa polisi wawili.

Wakati alipokuwa akitoa ujumbe wa Rais Paul Kagame kwenye makao makuu ya Polisi ilioko Kacyiru mjini Kigali, Waziri wa usalama wa ndani, Sheikh Musa Fazil Harerimna aliwapongeza wastaafu kwa kujitoa mhanga na kuhudumia nchi kwa nguvu zote ili kuimarisha usalama na hasa jeshi la polisi.

‘’Leo hii, sisi tunasherehekea nguvu, uadilifu na uzalendo mlioonesha kwa ajili ya kujenga nchi yenu.’’ Alisema waziri wa usalama.

‘’ Rais wa Rwanda awasifu kwa kujitoa mhanga na ahadi yenu kwa kujijengea nchi ya leo, chochote ambacho mtafanya baada ya kuacha majukumu ya kipolisi, mnatakiwa kuendeleza taasisi mliojenga.’’ Waziri Harerimana aliongeza.

‘’jukumu lako la kujenga taifa haina mwisho, badala nyinyi mnaelekea katika majukumu mengine, mnaacha jeshi lenye nguvu, na mkumbuke kwamba bado mko sehemu ya familia yenye ushindi na familia inayohitaji uwezo wenu.’’

Yeye alitoa wito hawa wastaafu kuendelea kuwa mfano wa kuigwa popote watakapo na kuendelea kuchangia uzoefu wao kwa kuendeleza nchi.

Waziri pia aliwashukuru wachumba wao na familia zao kwa uvumulivu wao, kusaidiana na kuungana mkono wakati wao walipokuwa wakihudumu jeshi la polisi.

Bi. Mary Gahonzire, aliyekuwa inspekta mkuu wa polisi na naibu mkuu wa taasisi ya huduma za kurekebisha Rwandab ni mmoja wa maafisa wa polisi waliostaafu

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments