Kiongozi wa Boko haram apinduliwa

Abubakar Shekau
Kundi la kigaidi linalojiita Islamic State siku ya jumatano lilichapisha tangazo lisemalo kwamba Abou Moussab al-Barnawi aliteuliwa mkuu mpya wa kundi la Boko haram linalofanya vitendo vya kigaidi nchini Nigeria na nchi majirani.

Katika ujumbe wa dakika kumi ambayo Abubakar Shekau aliyosambaza katika lugha ya kiarabu na kihausa, Shekau ambaye alikuwa mkuu wa kundi hilo alimshtaki Barnawi na wafuasi wake kujaribu kumpindua kwa kutuma taarifa za uongo kwa viongozi wa Islamic state walioko Mashariki ya kati.

‘’ wao waliniuliza kutuma itikadi yangu kupitia maandishi kwa Khalifa, lakini ujumbe ulikuwa kijanja kutokana na maslahi kibinafsi .’’ Shekau alisema.

‘’ shauri yao, sisi tutaendelea kupigana ili kuanzisha serikali ya Kiislamu.’’ Yeye ameyasema katika lugha ya kiarabu.

Kiongozi huo wa boko haram ambaye hakupatikana kwenye mitandao ya kijamii katika miezi ya karibuni, alisema alishangazwa na badala yake.

Kwa niaba yake, katika barua nane alizotuma kwa viongozi wa Islamic State alieleza utii wake na msimamao imara ambayo utabaki mpaka yeye kukatwa kichwa na alihakikisha kuzingatia mwenendo wa mwanzilishi kiroho baada ya kifo chake mwaka wa 2009.

Shekau alisema kwamba Abou Moussab al-barnawi na wafuasi wake ni washirikina.

Viongozi wapya wanamshtaki Shekau kukiuka itikadi mwanzilishi ya dhehebu hilo, kufukuza washauri waliotumwa na Islamic state, mashtaka ambayo Shekau alitupilia mbali.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments