Wakulima wa viazi wanalalamika hasara, Burera.

Baadhi ya wakulima wa viazi katika tarafa la Rugarama, Wilaya ya Burera, kasikazini mwa Rwanda wanalalamika hasara. Wao wanasema kwamba wana tatizo hatari la kukosa soko la mavuno yao na ni tatizo ambalo linaweza kuwa chanzo cha umaskini.

Hawa raia wa vijiji vya Karangara na Cyahi wanasema kuwa wao wanaishi kwa viazi lakini hawana wanunuzi kutoka mjini Kigali bali hawajui nini kilichowazuia kuja kama vilivyokuwa zamani au kwa nini hawakujengewa kiwanda cha kuzalisha viazi katika bidhaa nyingine.

Hawa raia wanasema kwamba kukosa wateja wanaotoka mjini au kiwanda husababishwa kununuliwa kwa bei nafuu.

Ntahonkiriye Felecien, raia wa Cyahi anasema kwamba hili tatizo linaendelea kupanda juu kwani hivi sasa bei ilishuka kwa 80 kutoka 150 Rwf kwa kilo.

‘’ tunataka mtusaidie kuuza viazi, kuna mavuno mengi na tunataka mtusaidie kupata soko na wanunuzi, na wao ambao wanakuja wanatununulia kwa bei ya mboga.’’ Ntahonkiriye alisema.

Hata hivyo uongozi wa Rugarama unasema kuwa hilo ni tatizo ndogo, Pierre Roger Dukuzumuremyi ambaye ni msimamizi wa maswala ya kijamii aliwahamisha raia kuhuhadhi mavuno na kuachana na wanunuzi wasio halali ambao wanawanunulia kwa be ya chini.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments