Rwanda kukosoa uamuzi wa Burundi wa kukata uhusiano wa kibiashara

Jumamosi iliyopita, SOS Media Burundi iliandika kwamba katika umuganda uliofanyika tarehe 30,Julai,2016 katika soko la Rugombo lilioko Cibitoke magharibi mwa Burundi, Joseph Butore ambaye ni makamu Rais wa pili nchini humo alitangaza kuwa hakuna mavuno za kilimo ambazyo yatauzwa nchini Rwanda kutoka Burundi.

Na alisisitiza kwamba mtu yeyote atakayekamatwa akisafirisha mavuno ya kilimo nchini Rwanda atachukuliwa adhabu kali.

Lakini waziri wa biashara na viwanda nchini Rwanda amekosoa uamuzi huo, Bw. Francois Kanimba anasema kwamba kuamua kukata uhusiano wa biashara utaathiri nchi hizo mbili majirani.

Kwanza, Kanimba amesema kuwa nchi kama Burundi mwanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki ni knyume na masharti ya biashara katika jumuiya na iwapo Rwanda kutaka, inaweza kuchukua Burundi mahakamani, lakini hataki.

‘’kiongozi katika nchi iliosaini makubaliano ya kibiashara ya jumuiya ya Afrika mashariki ni kinyume na sheria kusimama hadharani kisha ukajigamba kukata biashara, na ukitaka unaweza kutekeleza uamuzi kwa siri.’’
Kanimba amesema.

Yeye aliongeza kuwa Burundi ikiwa ikiendelea uamuzi wao, biashara kati ya Rwanda na Burundi itaathirika.

Kanimba anasema kuwa yeye alishangazwa na uamuzi wa uongozi wa Burundi kwani yeye hasikii jinsi nchi kama Burundi inayoendelea kukabiliwa na tatizo la uhaba wa pesa za kigeni huweza kuamua kukata mauzo ya nje.

Kanimba anafafanua uamuzi wa Burundi kama kupoteza soko kwa upande wa Burundi wakati Rwanda inaweza kutafuta mahali pengine pa kununua mavuno ya kilimo.

Yeye alifafanua kuwa baada ya ghasia kuzuka nchini humo, Rwanda ilipoteza soko ambalo lilianza kukua lakini si kitu kubwa ambacho unaweza kusema kitaathiri uchumi wa Rwanda.

Changia hii habari na wenzako.

Comments

Tumia Comments